Rais Sarkozy wa Ufaransa ziarani India | Habari za Ulimwengu | DW | 26.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Rais Sarkozy wa Ufaransa ziarani India

NEW DELHI:

India na Ufaransa zimetangaza mipango ya kupanua uhusiano wa nchi hizi mbili pamoja na kufungua ushirikiano wa nguvu za nuklia mapema sana India itakapo weza kuingia katika soko la kimataifa la nishati ya atomik.

Mjini New Delhi,waziri mkuu wa India,Manmohan Singh amesema kuwa amekubaliana na rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ,anaeizuri India kwa sasa ,kwenda mbele zaidi ya kile kinachoweza kuitwa uhusiano wa muuzaji na mnunuzi na Ufaransa.Aidha Sarkozy amesema kuwa majadiliano kuhusu mkataba wa vinu vya nguvu za Nuklia umekamilishwa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com