Rais George W. Bush wa Marekani atowa mkopo kunusuru kampuni za magari Marekani | Masuala ya Jamii | DW | 20.12.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Rais George W. Bush wa Marekani atowa mkopo kunusuru kampuni za magari Marekani

Rais George W. Bush wa Marekani ametowa mkopo wa dharura wa dola bilioni 17. 4 kuzinusuru kampuni kuu za magari nchini lakini hatima ya kampuni hizo inaelezwa kuwa iko mikononi mwa rais mteule wa Marekani Barack Obama.

default

Rais George W. Bush wa Marekani.

Bush amesema hapo jana kwamba kuziachilia kampuni hizo zisambaratike sio chaguo kutokana na nchi hiyo kukabiliwa na ushukaji wa uchumi wake, kuathirika kwa sekta ya nyumba na otowaji ovyo wa mikopo lakini pia ametaka kampuni hizo na wafanyakazi wake kuchukuwa hatua kali za marekebisho.

Bush anasema washauri wake kiuchumi wanaamini kwamba kusambaratika kwa kampuni hizo kutatowa pigo kubwa lilisilokubalika kwa Wamarekani wanaofanya kazi kwa bidii kupindukia sekta ya magari,kutaathiri zaidi soko dhaifu la ajira na kuufanya mgogoro wa fedha kuwa mbaya zaidi pamoja na kuzidi kuathiri uchumi kwa muda mrefu.

Bush amesema hali hiyo ingelifanya rais mpya kukabiliana na kuangamia kwa sekta kuu ya Marekani katika siku zake za kwanza madarakani.

Kampuni kuu za magari nchini humo za General Motors na Chrysler zimefurahia hatua hiyo na kuahidi kujenga upya sekta yao hiyo ambapo huko nyuma ilikuwa imara juu ya kwamba zimekiri kuwa itakuwa vigumu kuanza mwanzoni kabisa zikiwa kwenye ukingo wa kusambaratika.

Obama ambaye anaingia madarakani katika kipindi cha mwezi mmoja unaokuja amepongeza hatua hiyo ya serikali ya Bush lakini ameonya kwamba kampuni hizo za magari hazipaswi kuvuruga fursa hiyo ya kuzifanyia mageuzi hatua mbaya za uongozi.

 • Tarehe 20.12.2008
 • Mwandishi Mohamed Dahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GKIk
 • Tarehe 20.12.2008
 • Mwandishi Mohamed Dahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GKIk
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com