1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

George Weah

George Tawlon Manneh Oppong Ousman Weah, ni mwanasiasa wa Liberia anaehudumu kwa sasa kama rais wa 25 wa Liberia tangu Januari 2018, na mwanasoka mstaafu aliecheza katika nafasi ya ushambuliaji.

Baada ya kuanza maisha ya soka nyumbani kwao Liberia, Weah alitumia miaka 14 akivichezea vilabu vya nchini Ufaransa, Italia na England. Arsene Wenge ndiye alimleta Ulaya kwa mara ya kwanza, alipomsaini kwa ajili ya klabu ya Monaco mwaka 1988. Alijiunga na siasa za Liberia baada ya kustafu soka. Aliunda chama cha Alliance for Democratic Change na kuwania bila mafanikio, uchaguzi wa rais mwaka 2005, baada ya kushindwa na Ellen Johnson Sirleaf katika duru ya pili. Katika uchaguzi wa 2011, aligombea bila mafanikio, kama makamu wa Wiston Tubman. Weah hatimaye alichaguliwa katika bunge la seneti la Liberia, kuwakilisha kaunti ya Montserado katika uchaguzi wa 2014. Weah alichaguliwa kuwa rais wa Liberia katika uchaguzi wa 2017, baada ya kumshinda makamu wa rais Joseph Boakai, na kuapishwa Januari 22, 2018. Ukurasa huu ni mkusanyiko wa maudhui za DW kuhusu George Weah.

Onesha makala zaidi