1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Misri kuandamana upya leo

Thelma Mwadzaya28 Januari 2011

Raia wa Misri wanajiandaa kufanya maandamano makubwa zaidi hii leo yaliyo na azma ya kumshinikiza Rais Hosni Mubarak ajiuzulu baada ya kuwa madarakani kwa kipindi cha miaka 30.

https://p.dw.com/p/106K2
Vurugu za Cairo za JumatanoPicha: AP

Mwanasiasa muhimu wa upinzani,Mohamed El Baradei,ambaye ni kiongozi wa zamani wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Atomiki,IAEA,kwa sasa yuko nchini Misri ili kuwaunga mkono waandamanaji hao,baada ya kuuzuru mji wa Vienna ulioko Austria.Kwa mujibu wa mshindi huyo wa Tuzo ya Nobel,uongozi wa Rais Hosni Mubarak umewawia waMisri vigumu na kilichosalia ni maandamano.

Flash-Galerie Ägypten Mohamed El Baradei
Kiongozi wa IAEA wa zamani na mshindi wa Tuzo ya Nobel Mohamed El Baradei:yuko Misri kuwaunga mkono wapinzani wa Hosni MubarakPicha: AP

Mohamed El-Baradei anaaminika kuwa mgombea mtarajiwa atakayetoa ushindani mkubwa kwa rais Hosni Mubarak katika kinyang'anyiro cha kuwania urais mwaka huu. Wafuasi wa wanasiasa wa upinzani wamekuwa wakiandamana tangu siku ya Jumanne katika mji mkuu wa Cairo na Suez,ulio bandarini ijapokuwa wamepigwa marufuku.Kwa sasa kiasi ya watu alfu moja wamekamatwa na wengine 6 wameuawa kwasababu ya purukushani hizo.