QUITO : Mfuasi wa mrego wa shoto ashinda uchaguzi wa rais | Habari za Ulimwengu | DW | 27.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

QUITO : Mfuasi wa mrego wa shoto ashinda uchaguzi wa rais

Mfuasi wa sera za mrengo wa shoto Rafael Correa ambaye urafiki wake na kiongozi wa Venezuela anayeipinga Marekani Hugo Chavez na wito wake wa kupunguza malipo ya madeni ya kigeni kulikosababisha mashaka kwenye serikali ya Marekani inaonekana kuwa ameshinda kiulaini uchaguzi wa rais wa Ecuador ambao mpinzani wake anadai kuwa umehujumiwa.

Ushindi huo wa Correa utazidi kuimarisha mwelekeo wa Marekani ya Kusini kuelemea sera za mrengo wa shoto kwa Ecuador kujiunga na serikali za mrengo wa shoto za Venezuela,Bolivia,Brazil, Argentina na Chile.

Zaidi ya theluthi moja ya kura zikiwa zimehasabiwa Correa amejipatia asilimia 67.33 ya kura wakati mpinzani wake Alvaro Noboa amejipatia asilimia 32.67 ya kura.

Mtaalamu wa kiuchumi aliepata mafunzo yake nchini Marekani Correa amesema wameupokea ushindi huo kwa utulivu na unyenyekevu.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com