1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONGYANG:Viongozi wa Korea mbili wakamilisha mkutano wa siku mbili

5 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7IM

Viongozi wa Korea mbili za Kusini na kaskazini wamekamilisha mazunguzo yao ya siku tatu yaliyowezesha kutiwa saini makubaliano ya amani na biashara baina ya nchi zao mbili.

Marais Roh Moo Hyun wa Korea Kusini na Kim Jong IL wa Korea Kaskazini wamesema kwamba wataitisha mkutano na China na Marekani utakaojadili uwezekano wa kumaliza uhasama wao tangu vita vya mwaka 1950 hadi 53.

Viongozi hao pia wamekubali kuanzisha ushirikiano wa pamoja katika shughuli za uvuvi kufuatia mzozo wa mipaka katika eneo la pwani na vile vile kuanzisha huduma za treni zilizokatizwa wakati wa vita.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon amepongeza maafikiano hayo ya Korea zote mbili na ameahidi msaada wa umoja wa mataifa katika kufanikisha amani ya kudumu katika eneo hilo.