Prague.Rais Vaclav Klaus wa Jamhuri ya Czech amteuwa Mirek Topolanek kuwa Waziri Mkuu. | Habari za Ulimwengu | DW | 09.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Prague.Rais Vaclav Klaus wa Jamhuri ya Czech amteuwa Mirek Topolanek kuwa Waziri Mkuu.

Rais wa Jamhuri ya Czech Vaclav Klaus amemteuwa kiongozi wa chama cha mrengo wa kulia Mirek Topolanek kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo.

Hii ni mara ya pili kwa wanasiasa kutoka chama cha mrengo wa kulia kupewa nafasi hiyo tangu uchaguzi wa mwezi June, ulioliacha bunge katika hali ya mkwamo.

Topolanek anakabiliwa na kazi ngumu ya kuunda serikali itakayoweza kupata kura ya imani bungeni, huku makundi ya mrengo wa shoto na bawa la kati la mrengo wa kulia yakiwa na viti sawa- mia moja kila upande.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com