1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Weimar

Weimar ni mji ulioko katika jimbo la kati la Thuringia nchini Ujerumani. Umetoa mchango mkubwa katika historia na urithi wa Ujerumani

Pamoja na miji jirani ya Erfurt na Jena, Weimer inaunda sehemu ya eneo lenye wakaazi wengi jimboni Thuringia. Mji huo ulikuwa kitovu cha kutaalamika kwa Ujerumani, ambapo watu kama Goethe, Schillers na Franz Liszt walikuwa na makao yao mjini humo. Vuguvugu la usanifu ujenzi la Bauhaus liliasisiwa katika mji huo. Katiba ya kwanza ya kidemokrasia ya Ujerumani ilisainiwa mjini humo baada ya vita kuu vya kwanza vya dunia, na kipindi cha kati ya 1918 na 1933 kilijulikana kama Jamhuri ya Weimer nchini Ujerumani.