Polisi wazuia shambulio la bomu | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 25.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

IDHAA YA KISWAHILI

Polisi wazuia shambulio la bomu

---

ISTANBUL

Polisi nchini Uturuki wamefahamisha kwamba wamezuia shambulio la bomu katikati ya mji wa Istanbul na wamemkamata mtu anayetuhimiwa kuwa nyuma ya njama hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na afisa mmoja katika mji huo wa Istanbul mtu aliyekamatwa ni kijana mwenye umri wa miaka 25 na alikuwa amebeba zaidi ya kilo tatu ya miripuko na chombo cha kufyatulia kilichounganishwa na simu ya mkononi vilivyokuwa ndani ya mfuko.Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kwamba polisi walivamia nyumba moja ambako pia walipata miripuko zaidi na bidhaa nyingine za kutengenezea mabomu.Watu wengine zaidi pia walikamatwa kufuatia kisa hicho.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com