Paris.Watu watano wakamatwa kufuatia sakata la kuchomwa moto basi la abiria. | Habari za Ulimwengu | DW | 31.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Paris.Watu watano wakamatwa kufuatia sakata la kuchomwa moto basi la abiria.

Polisi nchini Ufaransa inawashikilia watu watano, watatu kati yao wanahusishwa na tukio la kulichoma moto basi huko mjini Marseille.

Katika tukio hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, lilipelekea kuungua vibaya mwanamke mmoja ambae hali yake imetajwa kuwa ni baya.

Polisi mjini paris wamesema, kamata kamata hiyo ilifanyika mapema leo asubuhi katika jumba la sinema karibu na mahali palipotokea tukio la kuchomwa moto basi hilo lililokuwa na abiria.

Kuchomwa moto kwa basi hilo, kumewashtua sana wanasiasa na wananchi nchini Ufaransa.

Hapo jana waziri mkuu wa Ufaransa Dominique de Villepin alitangaza mpango wa hukumu ya kifo kwa yeyote atakae husika na maafa kama ya uchomaji moto basi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com