Paris. Baraza la mawaziri lina wizara 15 tu Ufaransa. | Habari za Ulimwengu | DW | 19.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Paris. Baraza la mawaziri lina wizara 15 tu Ufaransa.

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amezindua baraza lake la mawaziri lenye wizara 15 na kujumuisha wanawake saba.

Miongoni mwa uteuzi mkuu ni pamoja na msoshalist Bernard Kouchner kuwa waziri wa mambo ya kigeni.

Kundi lake lilitangazwa siku moja baada ya rais huyo kumteua Fillon kuwa waziri mkuu ambaye ataongoza kasi yake ya mageuzi.

Baraza hilo la mawaziri limepunguzwa kutoka mawaziri 30 chini ya utawala wa rais Jacques Chirac. Baraza hilo la mawaziri la Sarkozy limeingia katika historia kwa kuwa nusu ya mawaziri ni wanawake ikiwa ni pamoja na kwa mara ya kwanza kuwa na waziri mwenye asili ya Afrika kaskazini.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com