NEW YORK:Rais wa Iran aziuiwa kutembelea eneo la shambulizi la Sept 11 | Habari za Ulimwengu | DW | 20.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK:Rais wa Iran aziuiwa kutembelea eneo la shambulizi la Sept 11

Mamlaka ya jiji la New York imekataa kutoa ruhusa kwa Rais Mahmoud Ahmednejad kutembelea eneo la kituo cha biashara cha kimataifa kilichosambaratishwa na shambulizi la kigaidi la Septemba 11 mwaka 2001.

Rais huyo wa Iran aliomba atembelee eneo hilo wakati atakapokuwa mjini New York kuhudhuria kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wiki ijayo.

Msemaji wa Polisi wa New York amesema kuwa wamekataa kutoa ruhusa kwa kiongozi huyo wa Iran kutembelea eneo hilo kwa sababu za kiusalama.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Zalmay Khalilzad amekubaliana na uamuzi huo na kuilaumu Iran kwa kuunga mkono makundi ya kigaidi nchini Iraq, Lebanon na Afghanistan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com