1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Ban ateuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa

10 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4L

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limemteua waziri wa mambo ya nje wa Korea ya Kusini bwana Ban Ki Moon kuwa katibu Mkuu mpya wa Umoja huo. Bwana Ban anatarajiwa kuchukua nafasi ya Kofi Annan anaemaliza muda wake mnamo mwezi wa desemba.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linatazamiwa kuidhinisha uteuzi wa bwana Ban baadae wiki hii.