NEW YORK: Venezuela inakataa kugombea kiti katika baraza la usalama | Habari za Ulimwengu | DW | 18.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Venezuela inakataa kugombea kiti katika baraza la usalama

Venezuela inakataa kuwachilia kugombea kiti cha Latin Amerika katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Baada ya siku mbili na raundi 22 za upigaji kura, Venezuela haijashinda raundi hata moja dhidi ya Guatemala.

Lakini Guatamela imeshindwa kupata thuluthi mbili ya kura inazotakikana kushinda.

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa litapumzika kupiga kura leo na kuanza kupiga kura tena hapo kesho.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com