NEW YORK: Ushindani mkubwa kuliwakilisha eneo la Latina Amerika katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa | Habari za Ulimwengu | DW | 17.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Ushindani mkubwa kuliwakilisha eneo la Latina Amerika katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa

Hadi sasa kiti cha muakilishi wa eneo la Latina Amerika katika Baraza la usalama la Umoja wa mataifa kimesalia tupu baada ya kutopatikana mshindi kati ya Guatemala na Venezuela zilizokuwa zikiwania nafasi hiyo. Baada ya raundi 10 za kura, hakuna aliyepata theluthi mbili za kura zinazohitajika. Kura imepangwa kupigwa tena leo. Kura hiyo imegeuka ushindani mkubwa kati ya Marekani na rais wa Venezuela Hugo Chavez, ambae amekuwa akijaribu kutafuta uungwaji mkono katika nchi za Ashia, Afrika na Mashariki ya kati ili kukabiliana na maslahi ya Marekani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com