New York. Umoja wa mataifa waukaribisha uamuzi wa Rwanda kuondoa hukumu ya kifo. | Habari za Ulimwengu | DW | 28.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

New York. Umoja wa mataifa waukaribisha uamuzi wa Rwanda kuondoa hukumu ya kifo.

Kamishna wa haki za binadamu wa umoja wa mataifa ameukaribisha uamuzi wa Rwanda wa kufuta adhabu ya kifo. Louise Arbour ameisifu nchi hiyo kwa kuonyesha uongozi kwa vitendo, kutokana na kutangaza hatua hiyo siku ya Alhamis.

Uamuzi huo una maana pia kuwa zile nchi ambazo zimekataa kuwakabidhi watuhumiwa wa mauaji ya halaiki kwa mahakama nchini Rwanda kwasababu wanaweza kuhukumiwa kifo wanaweza sasa kufanya hivyo.

Umoja wa Ulaya pia umekaribisha hatua hiyo ukisema kuwa ni hatua muhimu kuelekea maridhiano katika nchi hiyo miaka 13 baada ya kutokea mauaji ya kimbari na watu zaidi ya 800,000 Watutsi na Wahutu kuuwawa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com