1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK . Umoja wa Mataifa wataka kuachiliwa wanamaji

30 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEF

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea wasi wasi wake mkubwa hapo jana kutokana na hatua ya Iran kuwashikilia wanamaji 15 wa Uingereza na kutowa wito wa kuachiliwa huru kwao pamoja na kufikiwa na mapema ufumbuzi juu ya utata wa suala.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari ambayo ilijadiliwa kwa zaidi ya masaa manne na kupunguzwa makali kutoka rasimu halisi ya Uingereza baraza hilo pia limeiomba Iran kuruhusu wanamaji kuwa na mawasiliano ya kibalozi.

Uingereza imeshindwa kuungwa mkono na Urusi iliokuwa ikiungwa mkono na Afrika Kusini na Indonesia kwa kutaka kutolewa kwa taarifa kali ambayo ingelilaani hatua hiyo ya Iran ya kuwashikilia wanamaji wake na kutaka kuachiliwa kwao mara moja.

Uingereza inasema wanamaji hao walikuwa katika eneo la bahari la Iraq katika operesheni ya kupiga vita magendo wakati Iran ikisisitiza kwamba walikuwa wameingia katika eneo la bahari yao.