NEW YORK: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aitaka Sudan kuchunguza bughdha iliyotendwa dhidi ya wafanyikazi wa Umoja huo. | Habari za Ulimwengu | DW | 25.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aitaka Sudan kuchunguza bughdha iliyotendwa dhidi ya wafanyikazi wa Umoja huo.

Uchumi unaendelea kuboreka nchini Ujerumani

Uchumi unaendelea kuboreka nchini Ujerumani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon ametoa wito kwa serikali ya Sudan kuchunguza kitendo cha juma lililopita cha kukamatwa na kujeruhiwa wafanyakazi 20 wa Umoja huo wanaotoa misaada katika eneo la Darfur.

Ban Ki-Moon amesema maafisa wa usalama wa Sudan waliwavamia na kuwakamata wafanyikazi hao katika mji wa Nyali, kusini mwa Darfur.

Makao ya Umoja huo nchini Sudan yamearifu baadhi ya wafanyi kazi hao walijeruhiwa wakati waliposhikiliwa kwa muda.

Umoja wa Mataifa umesema utawasilisha rasmi malalamishi kwa serikali ya Sudan kwa kukiuka sheria za kimsingi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com