NEW YORK : Azimio la haki za watu asilia laidhinishwa | Habari za Ulimwengu | DW | 14.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK : Azimio la haki za watu asilia laidhinishwa

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura kuidhinisha azimio la haki kwa ajili ya watu milioni 370 wa makabila asilia duniani.

Nchi 143 zimeunga mkono azimio hilo wakati nchi nne za Canada, Marekani,Australia na New Zealand zimepinga azimio hilo ambalo halizifungi nchi kisheria kwa kusema kwamba litawawezesha watu wa makabila hayo ya asilia kutumia kura ya turufu dhidi ya usimamizi wa taifa wa rasilmali.

Azimio hilo lililopitishwa kufuatia mjadala wa zaidi ya miaka 20 linasema wananchi wa makabila asilia wana haki wa kujiamulia mambo yao wenyewe, kudhibiti ardhi yao na rasilmali zao pamoja na kuwepo kwa kununi za kimataifa kushughulikia masuala yao.

Katika nchi kama vile Canada na Bolivia taratibu za maisha za watu asilia zimekuwa hatarini kutokana na uchimbaji wa madini, ubinafsishaji na uharibifu wa mazingira.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com