NEW DELHI:India yafanya jaribio la kombora la masafa mafupi | Habari za Ulimwengu | DW | 05.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW DELHI:India yafanya jaribio la kombora la masafa mafupi

India imefanya jaribio la kombora la masafa mafupi katika jimbo la mashariki la Orissa.

Hii ni mara ya nne kwa India kufanya jaribio la makombora yake ya masafa mafupi ya aina ya Agni -1 tangu mwaka 2002.

Kombora hilo la Agni- 1 lina uwezo wa kubeba kichwa cha nyuklia chenye uzani wa tani moja na linaweza kupiga umbali wa kilomita 700.

India na nchi jirani yake ya Pakistan mara kwa mara huwa zinatekeleza majaribio ya makombora kwa sharti kwamba zinaarifiana kabla.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com