NDJAMENA : Mkuu wa majeshi ya Chad auwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 30.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NDJAMENA : Mkuu wa majeshi ya Chad auwawa

Mkuu wa majeshi ya Chad auwawa katika mapambano makali na waasi karibu na mpaka na Sudan hapo jana.

Waziri wa Ulinzi Bichara Issa Djadallah amedai ushindi katika mapigano hayo ya jana na amesema kwamba zaidi ya waasi 100 wameuwawa baada ya vikosi vya serikali kupambana na msafara wa magari ya waasi ambao walikuwa wameiteka kwa muda miji miwili ya Chad wiki hii.

Kifo cha Generali Moussa Sougui ni pigo kubwa kwa Rais Idriss Derby anayepigwa vita na kimetokea ikiwa ni miezi michache tu baada ya waasi kumuuwa mpwa wake na mkuu wa majeshi Brigedia Generali Ababar Youssouf Mahamata Itno hapo mwezi wa Machi.

Jeshi la Chad limekuwa likidhoofika kutokana na mtiririko wa uasi wa wanajeshi wake na uhusiano kati ya nchi hiyo na Sudan umekuwa wa mvutano.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com