Ndege za NATO zalenga mji mkuu wa Libya | Matukio ya Kisiasa | DW | 14.05.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Ndege za NATO zalenga mji mkuu wa Libya

Ndege za jumuiya ya kujihami ya NATO zimeendelea kuushambulia mji mkuu wa Libya, Tripoli.

default

Kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi

Hiyo jana, NATO ilituhumiwa na serikali ya Muammar Gaddafi mjini Tripoli, kuwa imesababisha vifo vya viongozi 11 wa kidini wa Kiislamu katika shambulio la anga lililolenga mji wa mafuta Brega. Mji huo unadhibitiwa na vikosi vya Gaddafi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Franco Frattini amesema, Gaddafi amejeruhiwa katika shambulio jipya lililoilenga nyumba yake na kiongozi huyo huenda hayupo tena mjini Tripoli. Wakati huo huo, televisheni ya taifa ya Libya imetangaza kanda, yenye sauti ya Gaddafi, akisema kuwa yeye ni mzima na yupo mahala ambapo NATO haitoweza kumpata.

Wakimbizi wamiminika Italia

Migrants receives assistance as they arrive on the tiny island of Lampedusa, Italy, early Sunday, May 8, 2011. Italian police and coast guard officials on Sunday rescued some 400 illegal migrants coming from Libya whose boat was tossed against rocks near port in southern Italy after the steering malfunctioned, officials said. Tens of thousands of migrants have fled unrest in northern Africa since January, most arriving at Lampedusa, the nearest Italian port to Africa. (AP Photo/Francesco Malavolta)

Wakimbizi kisiwani Lampedusa

Wakati huo huo, wakimbizi wanaendelea kumiminika kusini mwa Italia wakitokea Libya. Kwa mujibu wa walinzi wa pwani wa Italia, takriban wakimbizi 1200 wamewasili kwa boti katika kisiwa cha Lampedusa kilicho katika Bahari ya Mediterania. Takriban wahamiaji hao wote, ni watu waliokimbia Libya hata kabla ya mapigano kutokea nchini humo. Ripoti zinasema kuwa boti zingine zimeonekana baharani zikiwa na wakimbizi.

Inatathminiwa kuwa hadi wakimbizi 11,000 wametua kisiwani Lampedusa, tangu mapambano kuzuka kati ya kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi na waasi wa Libya wanaoungwa mkono na jumuiya ya kujihami ya NATO. Kisiwa cha Lampedusa kina ukubwa wa kilomita 20 za mraba na ni kiasi ya kilomita 130 tu kutoka Tunisia.

 • Tarehe 14.05.2011
 • Mwandishi P.Martin/rtre/afp
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/RNuT
 • Tarehe 14.05.2011
 • Mwandishi P.Martin/rtre/afp
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/RNuT
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com