Nawaz Sharif aapa kuuangamiza utawala wa kiimla Pakistan | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 26.11.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Nawaz Sharif aapa kuuangamiza utawala wa kiimla Pakistan

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Nawaz Sharif, ameapa kufanya kila awezalo kusaidia kuuangamiza utawala wa kiimla nchini Pakistan.

default

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Nawaz Sharif, akilakiwa katika uwanja wa ndege wa mjini Lahore

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Nawaz Sharif, ameapa atasaidia kuuangamiza utawala wa kiimla nchini Pakistan.

Kiongozi huyo amesema atawasilisha hati yake ya uteuzi ili aweze kugombea katika uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 8 mwezi Januari mwakani.

Hata hivyo Nawaz Sharif, aliyerejea jana nchini Pakistan kutoka uhamishoni nchini Saudi Arabia, ametishia kuugomea uchaguzi huo iwapo rais Pervez Musharraf hataondoa utawala wa hali ya hatari.

Amesema amerejea nchini Pakistan kuwahudumia wanananchi na kuliokoa taifa. Wafuasi wake wanaamini yeye ndiye kiongozi pekee anayeweza kuikoa Pakistan.

Kurejea kwa Nawaz Sharif, aliyetimuliwa na rais Musharraf miaka minane iliyopita, kunaongeza shinikizo dhidi ya jenerali Musharraf amalize utawala wa hali ya hatari nchini Pakistan.

 • Tarehe 26.11.2007
 • Mwandishi Josephat Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CT3E
 • Tarehe 26.11.2007
 • Mwandishi Josephat Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CT3E
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com