Mzozo wa Zimbabwe | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 05.12.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Mzozo wa Zimbabwe

Mugabe anatishia kuitisha uchaguzi kabla ya wakati pindi mazungumzo yakishindwa

default

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe
Rais Robert Mugabe  amesema ataitisha uchaguzi wa mapema iwapo makubaliano ya kugawana madaraka na upinzani hayatafanikiwa katika muda wa miaka miwili ijayo. Kwa upande mwingine  Marekani imetoa msaada wa dolla  elfu 600  kwa zimbabwe ili kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu ambao umesasabisha  vifo ya mamia ya wazimbabwe katika muda wa wiki chache zilizopita.


Hatua ya marekani kutoa msaada huo wa kifedha, imetokana na  ombi la zimbabwe la kutaka  msaada wa kimataifa  baada ya kutangaza ugonjwa wa kipindu pindu ambao umesababisha  vifo vya  zaidi ya watu 560 kuwa janga la kitaifa.


Katika taarifa  shirika la misaada ya maendeleo la marekani USAID, limesema  pesa hizo zitatumika katika kukabiliana na  kuzuka kwa ugonjwa huo.


Msaada huo na shirika hilo, unafikisha  kiasi cha fedha zilizotolewa  na marekani kwa zimbabwe kutokana na uhaba wa chakula na pia kuisadia secta yake ya afya  kuwa zaidi ya dolla  millioni 220  tangu october mwaka jana..


Naibu msemaji wa wizara ya nje ya marekani Robert Wood aliwaambia wanahabari kuwa marekani inafwatilia kwa makini matukio nchini zimbabwe kuanzia  secta ya afya, kiuchumi na hata hali ya kisiasa.

Kwa mara nyingine aliitaka serikali  ya rais Mugabe kutekeleza  makubaliano ya kugawana madaraka na upinzani. Akinukuliwa na gazeti  linalomilikiwa na serikali la The Herald rais Mugabe naye amesema iwapo  makubaliano hayo hayatafanikiwa  katika muda wa miaka miwili ijayo basi  itabidi kufanywa kwa uchaguzi mkuu wa mapema. Rais mugabe  alisema na namnukuu…“tulikubaliana  kuupa upinzani wizara 13 huku tukigawana wizara  ya mambo ya ndani. lakini iwapo makubaliano hayo yatafeli katika muda wa mwaka mmoja unusu au miaka miwili ,basi itatubidi kufanya tena uchaguzi',mwisho wa nukuu.


Serikali ya rais Mugabe  imekabiliwa na panda shuka nyingi tangu alipopoteza katika raudi ya kwanza ya uchaguzi mkuu wa mwezi marchi, na kisha baadaye kujitangaza mshindi katika raundi ya mwisho ya uchaguzi huo uliosusiwa na  na kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai.


Hali mbaya ya miundo msingi imesadia kufanikiwa kuenea kwa haraka kwa ugonjwa wa kipundupindu huku zaidi za visa elfu 12 vikiripotiwa.


Uingereza  nayo imetangaza kutoa msaada wa dolla millioni 14.7 kwa Zimbabwe.Waziri mkuu wa uingereza Gordon Brown alimshutumu rais Mugabe kutokana na kuendelea kuzorota kwa hali nchini zimbabwe.Waziri mkuu wa kenya Raila Odinga naye amezitaka serikali za afrika,kuchukua hatua zitakazomuondoa madarakani  rais Robert Mugabe.


Matamshi hayo ya Raila  yanawadia  baada ya kufanya mashauri na  kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai ambaye amekuwa akizuru mataifa mbalimbali  ya bara uropa na afrika katika haraka za kutaka kuungwa mkono.Rais Mugabe na Tsvangirai  walitia saini makubaliano ya kugawana madaraka  zaidi ya  miezi mwili iliyopita,lakini wamekosa kukubaliana njisi  ya kubuni serikali ya  umoja wa kitaifa.


Askofu mkuu  wa afrika kusini Desmond Tutu  pia yumo katika orodha ya wale wanaotaka rais Mugabe kuondolewa kwa lazima  madarakani.


Wakati huo huo afrika kusini  wiki ijayo itawatuma viongozi wake wakuu serikalini nchini Zimbabwe ili kutathimi hali ya chakula ilivyo. • Tarehe 05.12.2008
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/G9rQ
 • Tarehe 05.12.2008
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/G9rQ
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com