Mzozo wa Fedha wagubika Mkutano wa Davos | Matukio ya Kisiasa | DW | 28.01.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mzozo wa Fedha wagubika Mkutano wa Davos

Mkutano wa Kiamatifa wa Uchumi unaofanywa Davos Uswisi, mwaka huu umegubikwa na mzozo wa fedha.Viongozi wa nchi na wanauchumi wapatao kama 2,500 wanahudhuria mkutano huo wengi wakionya itachukua miaka kuunyanyua uchumi.

Chinese Premier Wen Jiabao smiles as he arrives at the World Economic Forum in Davos, Switzerland on Wednesday Jan. 28, 2009. Business participants will search for solutions to the financial crisis with some 40 world leaders, but without the top finance officials of the new U.S. administration who are occupied by the crisis or by the confirmation process at home. (AP Photo/Michel Eule

Waziri Mkuu wa China Wen Jiabao akiwasili kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi Davos,Uswisi.

Mawaziri Wakuu Wen Jiabao wa China na Vladimir Putin wa Urusi baadae leo hii watauhotubia mkutano wa Davos kueleza mipango yao kuhusu njia za kukabiliana na mzozo mbaya kabisa wa fedha kupata kushuhudiwa tangu miaka 80 iliyopita.Putin na Wen vile vile watakuwa na mazungumzo ya faragha kubadilishana mawazo vipi mataifa hayo makuu yanaweza kushirikiana kutenzua matatizo ya kiuchumi.Macho yote yanaikodolea China inayozidi kuwa na usemi katika uchumi wa kimataifa.Marekani haijawakilishwa na afisa wa ngazi ya juu katika mkutano huo wa Davos. Waziri Mkuu Putin alieilaumu Marekani kusababisha mzozo wa fedha duniani,amepanga kukutana na wawekezaji waliopigwa na bumbuazi na jinsi mzozo huo unavyoathiri uchumi wa Urusi.Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown waliutumia mabilioni ya Dola kupambana na uchumi uliodorora ni miongoni mwa kama viongozi 40 wa nchi na serikali watakaohotubia mkutano wa Davos.

Mkutano huo ukigubikwa na mzozo wa fedha,wanasiasa na wakuu wa kibiashara walioshtushwa mno na jinsi mzozo huo ulivyoathiri uchumi kote duniani wanasema,hakuna suluhisho rahisi kwa mzozo uliokwamisha ukuaji wa uchumi.Kwa maoni yao,serikali zitapaswa kutoa misaada mikubwa ya fedha kuchangamsha uchumi unaodorora.Hakuna matumaini ya kuufufua haraka uchumi,viongozi wengi wa kibiashara wakisema, uchumi utakua pole pole na huenda ikachukua hadi miaka mitatu kabla ya kuimarika.Wakati huo huo Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini Trevor Manuel amesema,nchi tajiri zinatoa fedha kwa mabilioni,bila ya kujua kile kitakachofanywa hasa na pesa hizo.Ameonya,kuna hatari kwa nchi hizo kuibuka kutoka mzozo wa fedha zikiwa na madeni makubwa mno.Nae katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan alipozungumza na waandishi wa habari alisema,ulimwengu unakabiliwa na mizozo mitatu inayohusiana - hali mbaya ya uchumi duniani,wasiwasi wa nishati na mabadiliko ya hali ya hewa.Ni dhahiri kuwa matatizo ya uchumi na fedha yamegubika juhudi za kushughulikia masuala mengine muhimu kama maeneo mbali mbali ya migogoro,mabadiliko ya hali ya hewa duniani,juhudi za kueneza demokrasia,kupunguza umasikini katika nchi zinazoendelea na kupambana na ubaguzi wa jinsia.

Mkutano wa Kiamatifa wa Uchumi unaofanywa Davos Uswisi katika milima ya Alps,mwaka huu umegubikwa na mzozo wa fedha ulioathiri ulimwengu mzima.Viongozi wa nchi na wanauchumi wapatao kama 2,500 wanahudhuria mkutano huo baadhi yao wakionya kuwa itachukua miaka kunyanyua uchumi unaodorora.

Mawaziri Wakuu Wen Jiabao wa China na Vladimir Putin wa Urusi baadae leo hii watauhotubia mkutano wa Davos kueleza mipango yao kuhusu njia za kukabiliana na mzozo mbaya kabisa wa fedha kupata kushuhudiwa tangu miaka 80 iliyopita.Putin na Wen vile vile watakuwa na mazungumzo ya faragha kubadilishana mawazo vipi mataifa hayo makuu yanaweza kushirikiana kutenzua matatizo ya kiuchumi.Macho yote yanaikodolea China inayozidi kuwa na usemi katika uchumi wa kimataifa.Marekani haijawakilishwa na afisa wa ngazi ya juu katika mkutano huo wa Davos. Waziri Mkuu Putin alieilaumu Marekani kusababisha mzozo wa fedha duniani,amepanga kukutana na wawekezaji waliopigwa na bumbuazi na jinsi mzozo huo unavyoathiri uchumi wa Urusi.Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown waliutumia mabilioni ya Dola kupambana na uchumi uliodorora ni miongoni mwa kama viongozi 40 wa nchi na serikali watakaohotubia mkutano wa Davos.

Mkutano huo ukigubikwa na mzozo wa fedha,wanasiasa na wakuu wa kibiashara walioshtushwa mno na jinsi mzozo huo ulivyoathiri uchumi kote duniani wanasema,hakuna suluhisho rahisi kwa mzozo uliokwamisha ukuaji wa uchumi.Kwa maoni yao,serikali zitapaswa kutoa misaada mikubwa ya fedha kuchangamsha uchumi unaodorora.Hakuna matumaini ya kuufufua haraka uchumi,viongozi wengi wa kibiashara wakisema, uchumi utakua pole pole na huenda ikachukua hadi miaka mitatu kabla ya kuimarika.Wakati huo huo Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini Trevor Manuel amesema,nchi tajiri zinatoa fedha kwa mabilioni,bila ya kujua kile kitakachofanywa hasa na pesa hizo.Ameonya,kuna hatari kwa nchi hizo kuibuka kutoka mzozo wa fedha zikiwa na madeni makubwa mno.Nae katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan alipozungumza na waandishi wa habari alisema,ulimwengu unakabiliwa na mizozo mitatu inayohusiana - hali mbaya ya uchumi duniani,wasiwasi wa nishati na mabadiliko ya hali ya hewa.Ni dhahiri kuwa matatizo ya uchumi na fedha yamegubika juhudi za kushughulikia masuala mengine muhimu kama maeneo mbali mbali ya migogoro,mabadiliko ya hali ya hewa duniani,juhudi za kueneza demokrasia,kupunguza umasikini katika nchi zinazoendelea na kupambana na ubaguzi wa jinsia.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com