″Mwenyekiti wa benki ku ya dunia si lazma awe Mmarekani″-inasema Australia | Habari za Ulimwengu | DW | 27.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

"Mwenyekiti wa benki ku ya dunia si lazma awe Mmarekani"-inasema Australia

CANBERRA:
Australia imejiunga na nchi zinazotaka atakaekabidhiwa wadhifa unaoachwa na Paul Wolfowitz kama mwenyekiti wa benki kuu ya dunia,asiwe raia wa Marekani.”Wengine pia wa kutoka nchi nyengine za dunia wanastahiki kukabidhiwa wadhifa huo”-amesema waziri wa fedha wa Australia Peter Costello.Australia inaunga mkono kikamilifu madai ya mataifa 20 tajiri kwa viwanda na yale yanayoinukia-G20,yanayotaka pawepo hali ya uwazi kabisa katika kuteuliwa wakuu wa benki kuu ya dunia na shirika la fedha la kimataifa IMF bila ya kuwepo masharti ni raia wa nchi gani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com