Mtuhumiwa wa shambulio la shule achiliwa | Habari za Ulimwengu | DW | 20.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mtuhumiwa wa shambulio la shule achiliwa

Waendesha mashtaka wa Ujerumani wamesema vijana wawili waliokuwa wanatuhumiwa kutaka kuwashambulia wanafunzi na walimu katika shule yao ya sekondari waliamuwa kutotekeleza mpango wao huo kabla ya polisi kujulishwa juu ya njama hiyo.

Hayo yamebainishwa na uchunguzi wa awali. Waendesha mashtaka katika mji wa magharibi wa Cologne wamemuachilia huru mtuhumiwa mwenye umri wa miaka 18 ambaye atapelekwa kwenye hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya ugonjwa wa akili. Mtuhumiwa mwenzake mwenye umri wa miaka 17 amejiuwa kwa kujirusha chini ya treni muda mfupi baada ya kuhojiwa na kuachiliwa na polisi.

Wanafunzi wenzao wa darasa waliwagutusha walimu baada ya kuwaona watuhumiwa hao wakichunguza picha za mauaji ya mwaka 1999 ya shule ya sekondari katika jimbo la Colorado nchini Marekani ambapo wanafunzi wawili waliwapiga risasi na kuwauwa wanafunzi wenzao 12 kabla ya kujiuwa wenyewe.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com