Mtazamo wa vyama vya upinzani nchini Tanzania kuhusu swala la Zimbabwe | Matukio ya Kisiasa | DW | 01.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mtazamo wa vyama vya upinzani nchini Tanzania kuhusu swala la Zimbabwe

Miito na shutuma zinazidi kutolewa juu ya kurudi tena madarakani rais Robert Mugabe huku Uingereza ikisema muswaada wa Umoja wa mataifa wa kuiwekea vikwazo zimbabwe umeshaandaliwa.

default

Rais Robert Mugabe akishiriki katika mkutano wa viongozi wa Afrika huko Sharm el-Sheikh, nchini Misri

Katika mkutano wa viongozi wa Afrika unaoendelea huko nchini Misri Umoja wa mataifa na viongozi wa Umoja wa Afrika wamemtaka rais Mugabe kukaa kwenye meza ya mazungumzo na mpinzani wake Morgan Tsvangirai kufikia makubaliano ya kisiasa.Wakati huohuo waziri mkuu wa Kenya ameutaka umoja huo wa Afrika kumuondoa mugabe katika jumuiya hiyo.Haya yote yamezungumzwa wakati waangalizi wa uchaguzi kutoka jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC wakitoa taarifa yao iliyosema kwamba uchaguzi haukuwakilisha imani ya wazimbabwe.waangalizi wa umoja wa Afrika nao wamesema uchaguzi haukufikia viwango vilivyowekwa na nchi 53 za jumuiya hiyo.

Chini ya mkutano huo wa viongozi wa Afrika unaoendelea nchini Misri Je wapinzani barani Afrika wanautazama vipi mzozo wa Zimbabwe?Nimezungumza na Dkt Sengendo Mvungi aliyewahi kuwa mgombea wa urais wa chama cha NCCR Mageuzi nchini Tz.Na kwanza alikuwa na haya ya kusema.
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com