1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpango wa uokozi wa rais Obama

Sekione Kitojo11 Februari 2009

Waziri wa fedha wa Marekani ameainisha mwelekeo wa nchi hiyo utakaoitoa kutoka katika mzozo mkubwa wa kiuchumi na fedha tangu wakati wa mporomoko mkubwa wa kiuchumi nchini humo.

https://p.dw.com/p/GrVu
Rais wa Marekani Barack Obama kulia na waziri wa fedha Timothy Geithner.Picha: picture-alliance/ dpa

Waziri wa fedha wa Marekani Tiimothey Geithner amekutana na waandishi habari na kutoa mwelekeo wa Marekani kujitoa kutoka katika mzozo mkubwa wa kiuchumi na fedha tangu wakati ulipotokea mporomoko mkubwa kabisa wa kiuchumi. Masoko ya hisa ya kimataifa yamepokea taarifa hiyo hata hivyo kwa kuvunjika moyo, kama ilivyokuwa mjini New York pamoja na masoko mengi kushuka baada ya Geiithner kutoa maelezo ya mpango huo wa uokozi.

Waziri huyo wa Fedha wa Marekani ameiweka wazi hali hiyo ya kifedha nchini humo kwa kusema.

Hii ni changamoto kubwa, ambayo imejaa utata, kuliko ilivyokuwa inafahamika hapo kabla.

Serikali ya Marekani haina kingine cha kuchagua ila kuendelea kupambana na changamoto hii, kupitia rasilmali zilizopo za kitaifa na kifedha ambazo kwa pamoja zinaweza kuzuwia kuvurugika kwa mfumo wa fedha. Mporomoko huu utatugharimu zaidi na kuliko mabilioni ya fedha ambayo tunayaingiza katika kuuokoa uchumi ambayo yanahitajika hivi sasa.

Tunafahamu kuwa gharama za kuporomoka kwa uchumi wetu itakuwa kubwa mno kwa familia na biashara na kwa taifa letu.


Serikali ya Marekani inataka kuzuwia kuporomoka kwa uchumi wa nchi hiyo kwa kutoa kiasi cha mara mbili ya fedha zinazotakiwa.

Baraza la Senet limeidhinisha mpango wa dola bilioni 800 ambao utaweza kuharakisha kutoa fedha kwa majimbo pamoja na kuunda nafasi nyingi za kazi. Ni mpango mkubwa kabisa wa kutengeneza nafasi za kazi katika historia ya Marekani. Lakini hata hivyo hatua hiyo pekee haiwezi kuwa dawa ya kuufufua uchumi. Pamoja na hayo mbali ya kazi lakini lazima ipatikane mitaji.

Waziri wa fedha wa Marekani anapambana katika sehemu mbili za mapambano kutimiza jukumu hilo. Mpango huu wa kichocheo cha uchumi kama dawa ya kuliokoa soko la kazi utakuwa na nafasi tu , iwapo utahusishwa katika mpango mkubwa wa uokozi katika mabenki.

Ni lazima tutoe mikopo kwa familia na wafanyabiasha .

Sharti la mafanikio yake, ni kwamba uchumi wa Marekani una nafasi ya kutoka katika mporomoko. Na kwa wakati huu mabenki ya Marekani ambayo yako katika hali ya kufilisika si sehemu ya ufumbuzi wa tatizo hilo, badala yake ni sehemu ya tatizo. Na zimekalia juu ya mlima wa hisa ambazo zinaingiza hasara, hali ambayo inaziingiza kila kukicha katika madeni zaidi.


►◄