1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Barack Hussein Obama

Barack Hussein Obama II ni mwanasiasa wa Marekani na rais wa 44 wa taifa hilo kubwa kabisaa kiuchumi na kijeshi duniani. Ndiye Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Afrika kushika wadhifa huo.

Obama aliezaliwa katika mji wa Honolulu, Hawai ni mhitimu wa chuo kikuu cha Columbia na shule ya sheria ya Havard – ambako alihudumu katika nafasi ya rais wa jarida la “Havard Law Review”. Obama alishinda uteuzi wa chama cha Democratic mwaka 2007, baada ya kampeni kali dhidi ya Hillary Clinton, na hatimaye kumshinda mgombea wa chama cha Republican John McCain katika uchaguzi mkuu mwaka 2008. Mwaka 2012 aliwania muhula wa pili dhidi ya mgombea mwingine wa Republican, tajiri Mitt Romney na kumgaragaza.

Onesha makala zaidi