MOSCOW: Waziri mkuu wa Israeli Ehud Olmert aiomba Rushia kuzuwia Iran isipate silaha za kinyuklia | Habari za Ulimwengu | DW | 19.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW: Waziri mkuu wa Israeli Ehud Olmert aiomba Rushia kuzuwia Iran isipate silaha za kinyuklia

Waziri mkuu wa Israeli Ehud Olmert, ameiomba Rushia kuzuwia Iran isipate silaha za kinyuklia. Olmert yuko mjini Moscow kwa mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo. Kabla ya kupokewa kwa mazungumzo na rais wa Rushia,Vladimir Putin, waziri wa Rushia wa mambo ya kigeni, Sergei Lavrov, amesema kuwa anahisi hakuna haja ya kuchukua hatua juu ya mpango wa kinyuklia wa Iran. Waziri mkuu wa Israeli, Ehud Olmert, pia amesema inafaa vikwazo vya silaha viwekewe Iran na Syria ambazo zinalisaidia kundi la wapiganaji wa Hezebollah nchini Lebanon ambao walipigana vita vya mwezi na nusu na Israeli miezi mitatu iliopita.

Mnamo siku zilizopita, Rushia ilitupilia mbali pendekezo hilo la vikwazo dhidi ya Iran na Syria.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com