1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW : Urusi yasitisha ushiriki Mkataba wa Majeshi

14 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBis

Urusi imesitisha ushiriki wake kwenye mkataba muhimu wa kupunguza wanajeshi wa kawaida katika bara la Ulaya chini ya agizo lililotiwa saini na Rais Vladimir Putin.

Agizo hilo linasitisha dhima ya Urusi katika Mkataba huo wa Vikosi vya Kawaida barani Ulaya ambao unaweka vikomo vya idadi ya silaha nzito zilizowekwa kati ya Bahari ya Atlantiki na milima ya Urals.

Urusi ilitishia kujitowa kwenye mkataba huo kwa kuyashutumu mataifa ya magharibi kwa kushindwa kuridhia nakala yake iliofanyiwa marekebisho iliosainiwa hapo mwaka 1999 kwa kuzingatia hali mpya halisi ya baada ya kipindi cha Vita Baridi.