MOGADISHU: Afisa wa polisi auwawa
29 Januari 2007Matangazo
Watu waliokuwa na silaha wamevishambulia vituo vya polisi mjini Mogadishu na kuwaua watu wawili akiwemo afisa mmoja wa polisi. Serikali ya mpito ya Somalia imeonya kwamba wapiganaji wa kiislamu waliotimuliwa mwezi uliopita kutoka mjini Mogadishu wameanza kujikusanya na kuitolea mwito jumuiya ya kimataifa ipeleke majeshi ya kulinda amani nchini Somalia.
Waziri mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi, ambaye majeshi yake yaliwafurusha wanamagambo wa mahakama za kiislamu kutoka Mogadishu, amesema thuluthi moja ya jeshi lake litaondoka kutoka Somalia katika kipindi cha siku mbili zijazo.