Mkutano wa mawaziri wa fedha wa Umoja wa Ulaya | Matukio ya Kisiasa | DW | 07.09.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Mkutano wa mawaziri wa fedha wa Umoja wa Ulaya

Vikwazo kwa wanachama wanaokiuka mapatano.

Wolfgang Schaeuble (CDU)

Wolfgang Schaeuble (CDU)

Dharuba ilioiipiga sarafu ya Euro hivi karibuni, sasa imetulia,lakini , Umoja wa ulaya na hasa waziri wa fedha wa Ujerumani Bw.Schaüble,wamevinjari kusukuma mbele mageuzi ya ya usimamizi wa shughuli za fedha ili kuimarisha zaidi yale makubaliano ya kuimarisha sarafu hiyo-makubaliano ya nakisi ya nchi zanachama wa Euro kutopindukia 3% ya pato la Taifa.

Madeni ya serikali zanachama yasipindukie kima cha 3% ya pato zima la taifa n dio makubaliano na yule atakaevuka kima hicho atazamie kuadhibiwa.Kanuni hii imetungwa na wanachama wenyewe wa Umoja wa Ulaya ili kuiimarisha sarafu yao ya Euro.Lakini, mara tu kuzuka msukosuko wa fedha na uchumi ulimwenguni,hakuna mwanachama yeyote alieheshimu kanuni hiyo.

Ugiriki imekaribia kima cha 13% katika madeni yake na kima takriban ni sawa na hicho nchini Ireland.Hatahivyo, hadi sasa hakuna mwanachama alieadhibiwa na hata Ugiriki, nchi ambayo ndio iliozusha msukosuko mapema mwaka huu msukosuko wa sarafu ya Euro kuyumba-yumba.

Ni kutokana na hatua za kuiokoa Ugiriki isizame kwenye madeni yake na sarafu yenyewe ya Euro ndipo masoko ya fedha yaliweza kutulia.Kwa muujibu wa Kamishna wa mambo ya sarafu wa Umoja wa Ulaya Olli Rehn,uzembe juu ya mapatano ya kuimarisha sarafu ya Euro ukomeshwe.

"Ni kama katika mchezo wa mpira. Mchezo hauendi barabara ikiwa wachezaji wake wanabishana na rifu kila inapotokea faoul.Ndio maana vikwazo, viwe moja kwa moja jambo la kawaida kwa kila anaevunja kanuni."

Hadi sasa, ilipasa wanachama wote kuamua juu ya vikwazo na hivyo, kizingiti kikawa kikubwa kukiuka.Shauri analotoa Bw.Rehn, ni kugeuza hali hiyo ya kupitisha maamuzi.Pawepo wingi wa kutosha tu kupitisha uamuzi wa kumwekea vikwazo mvunjaji kanuni hii .Kwa Ujerumani, waziri wake wa fedha Bw.Wolfgang Schäuble,anaitikia pendkezo la Bw.Rehn.

"Inatupasa kujifunza darasa la matokeo yaliopita miezi ya kwanza ya mwaka huu.Hali sasa ni nzuri mno kutokana na maamuzi tuliopitisha nusu ya kwanza ya mwaka huu,lakini, baadhi ya wakati inaongoza kidogo kudharau kutojifunza darasa lake .Kipindi kilichopita punde hivi kilikuwa cha mapumziko na sasa tunarejea kazini."

Kwa kufanyika mageuzi katika usimamizi wa matumizi ya fedha ndani ya Umoja wa Ulaya, Bw.Schaüble, hatazamii upinzani mpya baada ya waakilishi wa nchi zanacahama na Bunge kimsingi, kwisha afikiana hayo.

Mwaka ujao kwahivyo, patakuwapo Idara 3 za kusimamia fedha -moja itakayo simamia mabenki,nyengine mashirika ya bima na nyengine soko la hisa na pia kutakuwapo utaratibu wa kuonya na mapema kuzuka hatari.

Kuna lakini, upinzani kutoza kodi ya biashara za fedha miongoni mwa nchi za Umoja wa Ulaya.Wapinzani wa mfumo huo wanakariri tena na tena ni kodi itakayotozwa kote ulimwenguni, ndio inayoingia akilini,ama sihivyo, Umoja wa Ulaya, utapatwa na hasara mbele ya masoko mengine ya fedha yatakayonufaika.

Mwandishi: Hasselbach,Christoph(DW Brüssel)

Mfasiri: Ramadhan Ali

Mhariri:M.Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com