Mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya. | Matukio ya Kisiasa | DW | 07.11.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya.

Nchi za Umoja wa Ulaya kuwa na msimamo wa pamoja mjini Washington.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya kwenye mkutano maalumu juu ya mgogoro wa masoko ya fedha, uliofanyika mjini Brussels.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya kwenye mkutano maalumu juu ya mgogoro wa masoko ya fedha, uliofanyika mjini Brussels.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana juu ya hatua za kuchukua ili kukabiliana na mgogoro wa fedha ulioikumba dunia.Viongozi hao waliokutana mjini Bruessels leo wamekubaliana kuwasilisha mpango wa pamoja kwenye mkutano wa Washington utakaojadili mgogoro huo wiki ijayo.

Mpango huo utawasilishwa kwenye mkutano wa viongozi wa nchi tajiri na zinazoinukia mjini Washingon watakaojadili msukosuko uliopo kwenye masoko ya fedha duniani.

Akielezea juu ya mkutano wa viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya, kamishna wa masuala ya fedha na uchumi wa Umoja huo Joaquin Almunia amesema viongozi hao wameafikiana juu ya mtazamo wa pamoja watakaouwasilisha kwenye mkutano huo wa mjini Washington. Kamishna Almunia amesema viongozi wa nchi za Ulaya wanaitaka Marekani ifanye maguezi ya haraka ili kuepuesha kutokea mgogoro mwingine wa fedha.

Kwenye mkutano wao wa leo viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya pia walijadili juu ya njia za kuweka mfumo wa kutoa tahadhari za mapema ili kuepusha misukosuko mingine.


 • Tarehe 07.11.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FpRG
 • Tarehe 07.11.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FpRG
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com