Mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya 4 | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 20.06.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya 4

Wakuu wa nchi 27 za Umoja wa Ulaya wanaendelea kukutana mjini Brussels

default

Waziri mkuu wa Slovenia ambaye pia ni rais wa sasa wa Baraza la Umoja wa Ulya, Janez Jansa.

Wakuu wa serekali na nchi za Umoja wa Ulaya wanakuatana mjini Brussels, Ubelgiji, na juu kabisa katika ajenda ya mazungumzo yao wanayatafakari matokeo ya kura ya maoni iliopigwa katika Jamhuri ya Ireland ambapo wananchi wengi waliukataa mpango wa kuirekebisha Jumuiya hiyo, kama inavotakiwa na Mkataba wa Lisbon.


Mjini Brussels watu hawajuwi la kufanya. Wiki moja baada ya wapiga kura wa Ireland kuukataa Mkataba wa Lisbon, kwa bidii viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya sasa wanatafuta njia ya kujikwamua na mzozo huo. Lakini wanajiepusha kuweka mbinyo kwamba uamuzi upatikane papo hapo. Ripoti itakayokuwa na mapendekezo ya suluhisho angalau itatolewa katika mkutano wa kilele wa umoja huo hapo Oktoba, mwaka huu. Hivyo ndivyo alivosema waziri mkuu wa Slovenia, Janez Jansa, ambaye ndiye rais wa baraza la Umoja wa Ulaya.


" Ni mapema mno kuamua. Lazima tuwe na wakati wa kuyachambua mambo na kufikia uamuzi. Na ni wazi kwamba kwa sasa hatuwezi kuweka wakati.+


Macho katika mkutano huo yalielekezwa jana kwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Ireland, Brain Cowen, ambaye katika karamu ya chakula cha usiku na wakuu wenzake wa nchi za Ulaya, alitoa tathmini kutokana na kura ya HAPANA kwa Mkataba wa Lisbon. Wenzake yaonesha wako tayari kutoa muda kwa nchi yake itafakari. Waziri mkuu wa Luxembourg, Jean-Claude Junker, alisema lazima kauli ya watu wa Ireland iheshimiwe.


Insert: O- Ton Junker( dt.)


" Hakuna demokrassia kubwa na ndogo katika Ulaya. Pale Wafaransa wanaposema HAPANA , Jumuiya ya Ulaya inayumba. Na wananchi wa Ireland wanaposema HAPANA hata mara moja tusiwashangae na kutafakari."


Kansela Angela Merkel wa Ujerumani alionya juuya kuwachiwa muda mrefu wa kutafakari, kwani pale Wafaransa na Waholnazi walipoikataa katiba ya Ulaya mwaka 2005, ilichukuwa miaka miwili hadi Mkataba wa Lisbon kusukwa. Hali kama hiyo mara hii isiweko.


Kama Mkataba wa Lisbon utaweza kuanza kufanya kazi kabla ya uchaguzi wa bunge la Ulaya hapo Juni mwakani ni alama ya kuuliza. Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa amesema bila ya mkataba huo wa kuirekebisha Jumuiya ya Ulaya, jumuiya hiyo haiwezi kupanuliwa zaidi, hata Croatia haiwezi kuingizwa, jambo lililopangwa mwaka 2010. Pia nchi yeyote ambayo bado haijatoa kibali chake cha mwisho kwa Mkataba huo inatakiwa ifanye hivyo, bila ya kujali kwamba wananchi wa Ireland wameukataa. Kuna wasiwasi kama Jamhuri ya Cheki itaukubali mkataba huo. Rais wa nchi hiyo, Vaclav Klaus, tayari ametangaza kwamba mkataba huo umekufa. Lakini rais wa komisheni ya Umoja huo, Jose Barroso, alikuwa na maoni mengine:


Insert: O-Ton Barroso...


"Kila serekali ambayo imetia saini mkataba huo, makubaliano hayo, pia inawajibika kufanya kila kinachowezekana ili kwamba upate kibali cha mwisho. Ndio maana nina imani kwamba serekali zote zitaukubali mwishoni mkataba huo.+


Jana Mfalme Elizabeth wa Uengerea alitia saini yake ya mwisho kwa mkataba huo.


Viongozi wa Jumuiya ya Ulaya huko Brussels walitishia kuiwekea Sudan vikwazo vipya na vikali zaidi dhidi ya Zimbabwe. Walisema wameingiwa na wasiwasi sana na kuengezeka matumizi ya nguvu na vitisho huko Zimbabwe, kabla ya uchaguzi wa wiki ijayo. Pia waliwataka watawala wa kijeshi wa Myanmar wamuachie huru kiongozi wa vuguvugu la kidemokrasia katika nchi hiyo, Aung San Suu Kyi, na viongozi wengine wa kisiasa. • Tarehe 20.06.2008
 • Mwandishi Miraji Othman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/ENQw
 • Tarehe 20.06.2008
 • Mwandishi Miraji Othman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/ENQw
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com