1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa FAO kumalizika leo

Kalyango Siraj5 Juni 2008

Pesa zaidi zinahitajika ili kufanikisha usalama wa chakula duniani

https://p.dw.com/p/EE4D
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon (kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO )Jacques Diouf, mjini Rome, Italy, 04 June 2008.Picha: picture-alliance / dpa

Mkutano wa kimataifa kuhusu chakula ulioanza mapema wiki hii mjini Roma unamalizika leo alhamisi.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa ameitaka jamii ya kimataifa itafute kila njia kuona kama inakabiliana na mgogoro wa chakula na kusema kuwa pesa zaidi ya Euro billioni 13 zitahitajika kila mwaka kukabiliana na njaa.

Mwito wa jumuia ya kimataifa wa kukabiliana na njaa unakuja wakati mkutano kuhusu chakula unakaribia ukingoni hii leo.Wajumbe katika mkutano huo wa umoja wa mataifa wanatayarisha mkakati wa pamoja ili kukabiliana na mgogoro ambao unazidisha njaa duniani.Muswada jaribio wa tamko la pamoja ambao umeweza kutupiwa jicho na waandishi habari,unaotoa mwisho wa kuzidisha uzalishaji chakula,kupunguza vizuizi vya kibiashara pamoja na kufanya uchunguzi zaidi kuhusu suala la nishati mbadala.

Moja wa miito ya sasa ili kupunguza tatizo la chakula duniani inaelezwa na mkurugenzi mkuu wa shirika la chakula na kilimo dunaini Jacquis Diof,aliesema kuwa shirika hilo linahitaji $1.5 billioni kwa kipindi cha miaka mitano ijayo kugharimia mipango ya kupata chakula.

Shirika la FAO linasema kuwa bei ya vyakula imepanda mara dufu katika kipindi cha miaka mitatu.Mkuu wa Benki ya Dunia Robert Zollick amesema kuwa kupnda kwa bei ya vvyakula kumesababisha ghasia katika mataifa zaidi ya 30 dunaini.

Miongoni mwa watu hao waanaohitaji msaada ni wa kule kulikotokea ghasia za chakula kama vile Misri, haiti na mataifa mengie barani Afrika.Isitoshe mataifa kama vile Brazil,Vietnam, na India yamewekwa vizuizi dhidi ya kuuza nje chakula.

Ingawa wajumbe wote walikubaliana kuhusu usalama wa chakula lakini suala la nishati mbadala limekuwa tatanishi.

Wakosoaji wanahisi kumekuwa kama kuhepa suala hilo,wanasema muswada jaribio unasema kuwa nishati mbadala ni changamoto na wakati huohuo ni nafasi nzuri. Na kuongeza kuwa utafiti zaidi unahitajika.

Muswada huo unaendelea kusema kuwa uchunguzi zaidi unahitajika ili kuhakikisha kuwa uzalishaji pamoja na matumizi ya nishati mbadala ni wa manufaa kwa pande zote,huku ikitathminiwa kuwa kuna haja ya kuwa na chakula tosha duaniani.

Tamko kuhusu chakula linatarajiwa kutolewa leo alhamisi wakati wa kukamilishwa kwa mkutano wa chakula ambao umehudhuriwa na vigogo wengi dunia akiwemo rais Robert Mugabe wa Zimbabwe pamoja na rais wa Iran Ahmed Nejad.