Mkutano mkuu wa CDU kuanza mjini Hannover. | Matukio ya Kisiasa | DW | 02.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mkutano mkuu wa CDU kuanza mjini Hannover.

Mkutano mkuu wa CDU waanza mjini Hannover, ambapo chama hicho kinajiweka sawa kwa hali hapo siku za usoni.

Chama cha kansela Angela Merkel kinajiweka tayari kwa ajili ya hali ya hapo baadaye. Katika mkutano wake mkuu unaoanza leo Jumatatu hadi kesho Jumanne, chama cha Christian Democrats kinataka kutoa mpango mpya wa sera. Kinataka kama alivyosema katibu mkuu wa chama hicho Roland Pofalla kuwa katika miaka 15 hadi 20 ijayo chama hicho kinataka kutoa mwelekeo sahihi wa chama.

Zaidi ya mabadiliko 2,400 kuanzia msingi wa chama hadi ilani ya chama hicho pamoja na uongozi yatajadiliwa katika mkutano huo mkuu wa chama. Kwa hiyo kuna matarajio makubwa katika mkutano huo . Katika maoni ya wapiga kura chama hiki kinachoongozwa na kansela Angela Merkel kikiwa pamoja na chama ndugu katika jimbo la Bayern CSU kiko mbele. Kwa umbali mkubwa kinafuatia chama cha Social Democratic. Ili hali hiyo iendelee, chama cha Christian Democratic kinataka kujiweka katika nafasi ya kati katika mkutano wa chama hicho huko mjini Hannover. Kwa hiyo kauli mbiu ya mkutano huu ni Kushika mrengo wa kati. Chama cha Social Democratic , kama anavyoeleza katibu mkuu wa CDU Roland Pofalla kuwa katika mkutano wao mkuu mwishoni mwa mwezi Oktoba chama cha hicho kimejielekeza zaidi katika mrengo wa shoto.

O-Ton Pofalla.

Kama ilivyokuwa kwa mkakati wa Bwana Schröder katika chama cha Social democratic katika mkutano wao mjini Hamburg katika mwaka 1998 bila kuangalia mbali walijiwekea mkakati wa kuwa nguvu mpya ya mrengo wa kati , lakini bila ya kuwa na malengo na bila kuwa na wasi wasi na chama cha mrengo wa shoto chenyewe cha Linkspartei, wamejiweka katika pipa la taka , hii ninavyoona binafsi ni hatua ya kutiliwa maanani.

Chama cha CDU kinajiona kuwa ni mlinzi wa mageuzi ya Schröder, na wanataka, wakati wa uchaguzi mwingine baada ya miaka miwili waweze kupata wingi mkubwa wa kura. Upungufu mkubwa wa idadi ya watu wasio na kazi unathibitisha mwelekeo huo sahihi, anadai Pofalla.

Anasema kuwa maendeleo haya katika kupata nafasi nyingi za ajira hayafai kuchezewa. Ujerumani inahitaji mageuzi zaidi katika soko la kazi.

Na hilo linahitajika kuwamo katika ilani ya chama , ambapo wajumbe mjini Hannover watapaswa kuidhinisha. Lakini kwanza katika medani ya kisiasa CDU itabidi kujiweka katika nafasi ya kujadili zaidi suala la kuzuwia uhalifu , hususan mapambano dhidi ya ugaidi.

O-Ton Pofalla.

Imejitokeza hali , kwamba uwezo wa polisi katika katika matukio kama haya haujakuwa mkubwa. Ndio sababu ni lazima iwezekane kupata msaada wa jeshi katika masuala ya ndani , hususan katika hali ya hatari , kama tunavyotaka kuiweka katika ilani ya chama. Hii inatupa uhakika wa usalama kwa maisha na pia kuwa huru.

Chama cha Christian Democratic kimejiweka baina ya wahafidhina na waliberali katika suala la sera za kifamilia. Kutokana na vifungu hivyo katika ilani ya chama Pofalla anasema, kuwa hawataandika juu ya namna gani wazazi wanatakiwa kuwalea watoto wao. Wazazi wanatakuwa wawe huru , vipi wanaweza kuyashughulikia masuala ya familia na kazi.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com