1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkataba wa Lisbon waidhinishwa Bundestag

24 Aprili 2008

Bunge la Ujerumani-Bundestag limeuidhinisha leo mkataba wa mageuzi wa Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/Do7d
Kanzela Angela MerkelPicha: AP

Bunge la Ujerumani-Bundestag,limeidhinisha leo kwa wingi mkubwa Mkataba wa mageuzi wa Umoja wa Ulaya-mkataba wa Lisbon.Mkataba huo uliidhinishwa kwa kura 515 dhidi ya 58 zilizoupinga.Kwahivyo, umepitishwa kwa thuluthi-mbili ya kura zilizohitajika.

Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani,alionesha kuridhika mno kuona mkataba huo unaweza kuanza kazi Januari,mwakani baada ya wanachama wote 27 wa Umoja wa ulaya kuuidhinisha.

Ripoti ya Peter Stützle

Ni chama cha mrengo wa shoto tu (Link-partei) ndicho kilichoukataa mkataba huo .Kiongozi wa chama cha kiliberal (FDP) Guido Westerwelle alieleza hivi:

"kwa kweli ilikua bahati njema na bila kuamini kuona kwa mara ya kwanza katika historia yetu tunaishi katika nchi iliozungukwa na majirani walio marafiki,waliojikusanya chini ya paa moja la umoja wa Ulaya.Katika bara ambalo lilizowea vita kama jambo la kawaida,hii ni kama ajabu kubwa.Ni jambo la kufurahisha mno tulichojionea hapa."

Kwa kweli, Bw.Westerwelle, angelipendelea kuona kaTIBA HASA YA Umoja wa Ulaya inaidhinishwa na wananchi kupitia kura ya maoni,lakini mkataba wa Lisbon ni bora kuliko hali iliopo sasa ya kisheria.

Kisichomridhisha kwa vile aonavyo Bw.Westerwelle ni kuiona Ulaya inabakia kutozungumza kwa kauli moja katika maswali ya kilimwengu.

Aliongeza,

"Si uzuri kabisa, kuwa sisi Ulaya wakati huu,kuwaona wengine nje ya Ulaya, wamefaulu kutugawa tusizungumze kwa kauli moja katika maswali ya siasa za nje na ya usalama."

Bw.Westerwelle akigusia hapo kuridhia baadhi ya nchi zanachama wa Umoja wa Ulaya hukoUlaya ya mashariki kuwekwa makombora ya kujikinga -ambayo kwa jicho lake kunafufua mashindano mapya ya silaha.

Wazi kabisa zilikua ila alizotoa mwennyekiti wa chama kingine cha upinzani-chama cha mrengo wa shoto-Lothar Bisky:

"Mkataba huu wa mageuzi hautoi kamwe ishara ya amani .Uamuzi wa sera za usalama na za ulinzi wa pamoja umeachwa mikononi mwa majeshi.Tunahisi njia hii si barabara na ni ya hatari."

Mwenyekiti wa chama -tawala cha Social Democratic party (SPD) Kurt Beck ameungama kwamba mkataba wa Lisbon una kasoro ya jambo moja muhimu:

"Nacho ni kile tunachokiita Ulya ya wanyonge.Mkataba huu wa Lisbon hatahivyo unatoa fursa ya kurekebisha hayo.Na hapo ndipo ilipo tofauti na wale wanaoupinga mkataba huu."

Kwa mwenyekiti huyo wa SPD ni muhimu sana kuona Umoja wa Ulaya unasonga mbele na angependelea kuona mfano wa Ulaya unaigwa na sehemu nyengine za ulimwengu.

Hapo kabla, Kanzela angela Merkel alionesha kuridhika na matumaini ya kwamba kama ulivyopitishwa na Bunge la Ujerumani hii leo ,nchi nyengine zanachama wa Umoja wa Ulaya zitauidhinisha haraka ili uanze kazi januari mosi,2009.

"Ninawaambia wakati sasa umewadia kwa Ulaya,kwani miaka mingi tulikua tumejishughulisha sisi wenyewe.Kipindi cha kutokuwapo uhakika na cha kulemaa kimepita.Ni muhimu sasa tutupe macho usoni tunakokwenda."

Alisema Kanzela angela Merkel.