1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz: Putin anapigana 'vita ya mseto' dhidi ya Ujerumani

7 Oktoba 2025

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amemshutumu Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kuendesha "vita ya mseto" dhidi ya Ujerumani.

https://p.dw.com/p/51ZSh
Ujerumani Berlin 2025 | Kansela Friedrich Merz
Kansela Friedrich Merz 05.10.2025Picha: Uwe Koch/HMB Media/picture alliance

Merz aliambia kituo cha televisheni cha NTV hapa Ujerumani kwamba kiongozi huyo anapigana vita ya taarifa dhidi yao, anapigana vita ya kijeshi dhidi ya Ukraine na vita hiyo inawalengo wao wote.Aidha Kansela huyo wa Ujerumani aliongeza kwa kusema Putin anataka kuipindua kabisa hali ya kisiasa ya Ulaya na ndiyo sababu  wanaiunga mkono Ukraine. Anasema kwa maslahi ya Ujerumani  wanapaswa kulinda utaratibu wa kisiasa wa jamii zilizo wazi na huru barani Ulaya. Kansela Merz amesema kuwa alikuwa na mjadala mkali kuhusu suala hilo na Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orbán katika mkutano wa Umoja wa Ulaya uliofanyika Copenhagen juma lililopita.