Mateka wa Korea Kusini walemewa na maradhi | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 06.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Mateka wa Korea Kusini walemewa na maradhi

Kundi la Taliban latishia kuwauwa mateka zaidi wa Korea Kusini iwapo madai yao hayatatimizwa

Rais Hamad Karzai wa Afghanistan

Rais Hamad Karzai wa Afghanistan

Madakatari nchini Afghanistan wamewasilisha madawa kwa ajili ya mateka 21 wa Korea Kusini wanaozuiliwa na na kundi la Taliban kwa zaidi ya wiki mbili sasa.

Madaktari hao wamedondosha madawa hayo katika eneo la Ghazni linalomilikiwa na waasi.

Kundi la Taliban limetowa taarifa kuwa wengi kati ya mateka hao wa Korea Kusini wanauguwa wawili wakiwa katika hali mahututi. Kundi la Taliban limetishia kuwauwa mateka zaidi kutokana na kutokuwepo maendeleo yoyote katika majadiliano kuhusu mateka hao. Kundi hilo linataka serikali iwaachie huru wafungwa wa kundi hilo la waasi kutoka gerezani.

Serikai mjini Kabul hadi sasa imekataa kukidhi madai ya kundi la Taliban serikali hiyo inasema kukubali madai ya waasi ni sawa na kushawishi vitendo zaidi vya utekaji nyara. Rais Hamid Karzai ambae amewasili nchini Marekani kwa mazungumzo na rais Bush amesema serikali yake itafanya kila jitihada ili mateka hao waachiwe huru.

Viongozi hao wanatarajiwa kujadili hali ya usalama inayozidi kudidimia nchini Afghanistan na vitisho vya wapiganaji wenye msimamo mkali wanaojificha nchini Pakistan.

Wakati huo huo kamati ya dharura hapa nchini Ujerumani inaendelea na juhudi za kusaka uhuru wa mhandisi wa Kijerumani aliyetekwa nyara nchini Afghanistan.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com