1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaipa Ukraine hakikisho la ulinzi

16 Desemba 2025

Marekani imekubali kuipatia Ukraine hakikisho la usalama kama sehemu ya mpango wa kukomesha vita vya takribani miaka minne vya Urusi dhidi yake.

https://p.dw.com/p/55Pgv
Marekani, Trump, Zelensky
Rais Donald Trump wa Marekani (kushoto) ambaye nchi yake imetowa hakikisho la usalama kwa Ukraine.Picha: Tom Brenner/AFP/Getty Images

Maafisa wa Marekani wanaohudhuria mazungumzo kati ya nchi hizo mbili mjini Berlin, Ujerumani, walisema jioni ya jana kwamba hakikisho hilo, hata hivyo, linapaswa kukubaliwa kwa haraka.

Wajumbe wa serikali ya Marekani kwenye mazungumzo hayo, Steve Witkoff na Jared Kushner, wanaripotiwa kusema kwamba asilimia 90 ya mpango wa amani imekubaliwa na pande husika, na kwamba sasa wanatazamia kumalizia sehemu iliyobakia.

Hata hivyo, viongozi wa Ulaya wamelipokea pendekezo kwa hadhari licha ya kusifia hatua zilizopigwa kwenye mkutano huo wa Berlin.

Ukraine bado inasuasua kwenye kukubali pendekezo la Marekani la kuachia sehemu ya ardhi yake mikononi mwa Urusi ili kukomesha vita hivyo.