Mamilioni ya Walibya wahitaji msaada wa kibinaadamu | Matukio ya Afrika | DW | 18.05.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Mamilioni ya Walibya wahitaji msaada wa kibinaadamu

Umoja wa Mataifa unasema watu 2,100,000 wanahitaji msaada wa kibinaadamu kwa sababu ya mgogoro unaondelea nchini Libya kati ya vikosi vya waasi na vile vitiifu kwa kiongozi wa nchi hiyo, Kanali Muammar Gaddafi.

Muombolezaji mjini Misrata akilia mbele ya kaburi la jamaa yake

Muombolezaji mjini Misrata akilia mbele ya kaburi la jamaa yake

Mratibu wa Misaada wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, Panos Moumtzis, anasema watu wapatao 1,600,000 wanahitaji msaada kwa sababu mapigano yamevuruga huduma zote za msingi na kusababisha uhaba wa chakula na madawa.

Moumtzis anasema idadi hiyo ni pamoja na watu 460,000 walioyakimbia makaazi yao kwa sababu ya mapigano. Wengine 500,000 waliovuka mipaka kuingia Tunisia, Misri na kwengineko katika eneo hilo la Afrika Kaskazini, nao pia wanahitaji msaada.

Mjumbe huyo leo (18.05.2011) aliwaomba wafadhili wa kimataifa msaada wa dola milioni 408, kugharimia shughuli za misaada za Umoja wa Mataifa nchini Libya hadi kufikia mwezi Septemba mwaka huu.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman
Mhariri: Mohammed Khelef

DW inapendekeza