Waasi wa Libya ziarani Marekani | Matukio ya Kisiasa | DW | 14.05.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Waasi wa Libya ziarani Marekani

Marekani imeliita Baraza la Mpito la taifa la waasi wa Libya kuwa ni kundi la ''wapatanishi halali''.

default

Kiongozi wa Libya Moammar Gaddafi

Marekani hata hivyo, haikulipa kundi hilo hadhi ya kulitambua kidiplomasia baada ya mkutano na waasi hao wa NTC katika Ikulu ya Marekani jana. Waasi hao, wakiongozwa na kiongozi wao Mahmud Jibril wako mjini Washington Marekani kushinikiza kutambuliwa rasmi na kupata misaada zaidi ya kifedha.

Wakati huohuo, televisheni ya taifa ya Libya  ilirusha taarifa anayoripotiwa kuwa ni ya kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi, ambaye alikuwa akilaani shambulio la Alhamisi lililofanywa na majeshi ya NATO katika makaazi yake.

Tripolis NATO Luftangriff Gaddafi

Shambulio lililofanywa na jeshi la NATO, katika makaazi ya Gaddafi

Licha ya ripoti zilizotolewa awali kwamba kiongozi huyo wa Libya amejeruhiwa katika shambulio hilo, amesema katika taarifa yake kwamba hakudhurika na yuko katika sehemu ambapo mabomu ya majeshi ya NATO hayawezi kumfikia. Msemaji wa Gaddafi amesema kiongozi huyo bado yuko katika mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli.

 • Tarehe 14.05.2011
 • Mwandishi Halima Nyanza
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/11FyF
 • Tarehe 14.05.2011
 • Mwandishi Halima Nyanza
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/11FyF

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com