Malkia Elizabeth wa II afungua mkutano wa Jumuiya ya Madola | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 23.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Malkia Elizabeth wa II afungua mkutano wa Jumuiya ya Madola

Malkia Elizabeth II amefungua mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Madola katika mji mkuu wa Uganda,Kampala.Katika hotuba yake mbele ya marais na mawaziri wakuu waliokusanyika kwa mkutano wa siku tatu,Malkia Elizabeth alisema,jumuiya hiyo imewajibika kushughulikia matatizo ya wakati wetu.Hakuna jamii yo yote iliyokamilika na wala hakuna njia moja tu ya kupata mafanikio.

Rais wa Pakistan Jemadari Pervez Musharraf hakuwepo mkutanoni.Alkhamisi jioni,uanachama wa Pakistan ulisimamishwa baada ya Musharraf kushindwa kuondoa utawala wa hali ya hatari nchini mwake na kujiuzulu kama mkuu wa majeshi, kwa wakati aliowekewa na jumuiya hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com