1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamala kukutana na viongozi Ujerumani,Ufaransa na Uingereza

Lilian Mtono
16 Februari 2023

Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris anatarajiwa kukutana na kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron.

https://p.dw.com/p/4Nbb2
USA | Vizepräsidentin Kamala Harris
Picha: Senate Television/AP Photo/picture alliance

 Kamala Harris atakutana na viongozi hao atakapofanya ziara nchini Ujerumani na kuhudhuria mkutano wa masuala ya usalama mjini Munich. 

Kulingana na taarifa ya ikulu ya White House, Harris pia atakutana na kufanya mazungumzo namawaziri wakuu kutoka Finland na Sweden kuangazia mchakato wa mataifa hayo kujiunga na jumuiya ya kujihami ya NATO, lakini pia atazungumzia mahusiano na China katika mikutano na viongozi wa kigeni.

Soma pia:Blinken kuzuru Ulaya katikati mwa fukuto la mzozo na China

Makamu huyo wa rais pia atajadiliana kuhusu hatua zinazofuata kuhusu kuisadia Ukraine kwenye vita na mikakatiya kuiongezea mbinyo Urusi.