1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Blinken kuzuru Ulaya katikati mwa fukuto la mzozo na China

16 Februari 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken atahudhuria Mkutano wa Usalama wa Munich, ambapo mzozo na China, hofu ya mashambulizi mapya ya Urusi Ukraine na mkwamo na Uturuki kuhusu upanuzi wa NATO vitajadiliwa.

https://p.dw.com/p/4NY0O
USA | Antony Blinken
Picha: J. Scott Applewhite/AP/picture alliance

Waziri Blinken ataanzia ziara yake ya siku sita kwenye mkutano wa kimataifa wa usalama wa Munich, ambapo ataungana na Makamu wa Rais Kamala Harris kuwakilisha utawala wa Biden.

Uvumi ni mkubwa kwamba Blinken anaweza kutumia fursa hiyo kukutana na afisa mkuu wa sera ya mambo ya nje wa China Wang Yi ambaye pia atahudhuria mkutano wa Munich.

Hakuna mkutano kama huo umepangwa lakini ukifanyika yatakuwa mazungumzo ya kwanza ya ngazi ya juu na China tangu Blinken alipoahirisha safari ya China wiki iliyopita baada ya puto la China linaloshukiwa kuwa la ujasusi kudunguliwa katika anga la Marekani.

Soma pia: China yaishtumu Marekani kutumia nguvu baada ya puto lake kudunguliwa

Maafisa kadhaa wengine wa juu wa sera ya kigeni watahudhuria Mkutano wa Usalama wa Munich, mbali na wasiwasi unaoongezeka kuhusu shughuli za upelelezi za China, hali nchini Ukraine kuelekea mashambulizi yanayotarajiwa ya Urusi intarajiwa kuwa mada za majadiliano.

Chinas Spionageballon über den USA
Puto la China likielea kwenye anga la Marekani Februari 1, 2023 na kusaabisha mzozo mkubwa kati ya mataofifa hayo. Picha: Larry Mayer/Billings Gazette/AP/picture alliance

Mkutano huo unafanyika kuelekea mwaka mmoja tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, ambapo mkutano wa mwaka jana uligubikwa na maonyo kutoka Marekani na washirika wake wa NATO kwamba vita vilikuwa karibu.

Kutoka Munich, Blinken atasafiri hadi Uturuki, ambapo atapata fursa ya kuangalia shughuli za kutoa msaada na uokoaji kwa wahanga wa tetemeko la ardhi la wiki iliyopita, kabla ya kwenda Ankara kwa mazungumzo yanayotarajiwa na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na viongozi wengine wa juu.

Pingamizi la Uturuki dhidi ya Sweden

Moja ya vipaumbele vyake huko Ankara itakuwa kujaribu kuondoa pingamizi la Uturuki kwa Finland na Sweden kujiunga na NATO.

Erdogan amelalamika kwamba Wafinland na, haswa Wasweden, ni wapole sana kwa makundi ambayo Uturuki inayaona kuwa ya kigaidi au vitisho juu ya uwepo wake, yakiwemo makundi ya Kikurdi.

Erneuter Raketentest in Nordkorea im November 2022 - Reaktion Südkorea
Uturuki inataka Marekani iiuzie ndege za kisasa aina ya F-35.Picha: South Korea Defense Ministry/ZUMA Press Wire/dpa/picture alliance

Ili kuidhinisha wanachama wapya ndani ya NATO, mataifa yote wanachama yanapaswa kutoa ridhaa, na tayari mataifa yote 30 ukiacha Uturuki, yameridhia au kuashiria nia ya kuridhia kujiunga kwa Finland na Sweden.

Soma pia: Blinken akutana na Rais wa Misri kujadili mizozo ya kikanda

Wakati huo huo, Washington ina masuala mengine na Ankara, ikiwa ni pamoja na shauku ya Uturuki kununua ndege za kisasa za kivita za Marekani, jambo ambalo wabunge kadhaa wenye nguvu wanapinga kwa misingi ya haki za binadamu.

Blinken atamaliza ziara yake mjini Athens, ambapo atajadili mvutano unaoendelea kati ya Ugiriki na Uturuki, na masuala mengine, ikiwemo upatikanaji wa uhakika wa nishati katika eneo la mashariki mwa Mediterania na ushirikiano wa ulinzi.

Chanzo: Mashirika