1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yaishtumu Marekani baada ya puto lake kudunguliwa

6 Februari 2023

China imeishutumu Marekani kwa matumizi ya nguvu kiholela kufuatia kudunguliwa kwa puto lake linaloshukiwa kuwa la kijasusi. Beijing imesema hatua hiyo imeathiri vibaya juhudi ya pamoja katika kuleta utulivu wa uhusiano.

https://p.dw.com/p/4N9TK
Chinas Spionageballon über den USA
Picha: Larry Mayer/Billings Gazette/AP/picture alliance

Marekani ilidungua puto hilo la China kwenye pwani ya Carolina baada kuruka karibu na maeneo yake nyeti ya kijeshi. China imesisitiza kuwa tukio hilo lilitokea kimakosa na lilihusisha ndege ya kiraia.

China USA l stellvertretender Außenminister Xie Feng vor Gesprächen mit US-Vertretern
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Xie Feng (kulia).Picha: Phoenix TV/AP/picture alliance

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China Xie Feng amesema amewasilisha malalamiko rasmi katika Ubalozi wa Marekani siku ya Jumapili kuhusu kitendo cha Marekani kukishambulia chombo cha usafiri wa kiraia kisicho na rubani kwa kutumia nguvu za kijeshi.

Soma zaidi: Marekani yachunguza puto la Kijasusi la China kwenye angani

Uwepo wa puto hilo la China katika anga ya Marekani umeathiri pakubwa mahusiano ambayo tayari yamedorora kati ya mataifa hayo mawili ambayo kwa miaka kadhaa yamekuwa katika hali ya mvutano. Tukio hilo lilipelekea Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken kughairi ghafla ziara yake mjini Beijing ambayo ililenga kutuliza hali ya mivutano kati ya Beijing na Washington.

Soma zaidi:China yakasirishwa na hatua ya Marekani 

USA Abschuss chinesischer Ballon
Puto linaloshukiwa kuwa la China likidunguliwa na Marekani na kuelekea kuanguka baharini huko Carolina Kusini, 04.02.2023Picha: RANDALL HILL/REUTERS

China imesisitiza kuwa puto hilo lilikua la kiraia likiendesha utafiti kuhusu masuala ya hali ya hewa na liliingia katika anga ya Marekani kimakosa na kwamba wataendelea kuyalinda makampuni yao. Rais Joe Biden wa Marekani amesema aliamuru kudunguliwa kwa puto hilo kutoka umbali wa mita 18,000 lilipokuwa juu ya maji ili kuepuka madhara kwa raia walio nchi kavu.

Wabunge wa chama cha Republican walimkosoa siku ya Jumapili Rais Joe Biden kwa kusubiri siku kadhaa kabla ya kudungua puto hilo, wakimtuhumu kuonyesha udhaifu kwa China.

Matukio kama hayo kuripotiwa sehemu nyingine

USA Hagerstown | Joe Biden, Präsident | nach Abschuss chinesischer Ballon
Rais wa Marekani Joe Biden akiwasili katika uwanja wa ndege wa Hagerstown, Maryland 04.02,2023Picha: Andrew Caballero-Reynolds/AFP/Getty Images

Maputo kadhaa yanayoshukiwa au kuaminika kuwa ya China yameonekana huko Amerika ya Kusini hadi Japan. Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri la Japan Yoshihiko Isozaki amewaambia waandishi wa habari leo Jumatatu kwamba kifaa kinachoruka sawa na kile kilichodunguliwa na Marekani kilishuhudiwa angalau mara mbili kaskazini mwa Japan tangu mwaka 2020.

Soma zaidi: Marekani yaliona puto la pili la ujasusi la China

Washington na Beijing zimekuwa na tofauti kuhusu masuala mbalimbali kuanzia biashara hadi haki za binadamu, lakini China imekuwa ikikerwa zaidi na madai ya ukiukaji unaotolewa na Marekani kuhusu mamlaka katika maeneo yake. Beijing inapinga vikali mauzo ya kijeshi ya Marekani kwa Taiwan na ziara za wanasiasa wa kigeni katika kisiwa hicho, ambacho China inadai kuwa eneo lake ambalo inasema ikiwa itahitajika litarejeshwa kwa nguvu.