1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maji ni maada kuu kwa nchi za Afrika ya Mashariki

1 Julai 2011

Mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kuiingiza dunia katika machafuko makubwa, hasa baada ya dalili kujionyesha wazi kati ya Ethiopia na Misri, ambazo zimo kwenye mgogoro wa chini kwa chini kupigania umiliki wa Mto Nile.

https://p.dw.com/p/RX5A
Ramani ya Mto Nile
Ramani ya Mto NilePicha: CC/Lourdes Cardenal

Aliyekuwa mshindi wa tuzo ya Nobel na Rais wa zamani wa Misri, Anwar Saadat, aliwahi kuweka wazi kwamba maji ndio kitu pekee ambacho kitaifanya Misri iingie tena kwenye vita.

Imeelezwa kwamba, tishio hilo bado linabeba ukweli ikizingatiwa kwamba Ethiopia na Misri zote zipo pemebezoni mwa Mto Nile.

Ethiopia inapigania kupata sehemu kubwa ya mto huo, ambayo itawasaidia katika kuendesha shughuli za kilimo cha umwagiliaji na kuendeshea miradi ya umeme.

Ethiopia inaielezea hali ya sasa ya umiliki wa Mto Nile kama ya "kiza", kwani inatokana na sheria inayofuata taratibu ya enzi za ukoloni. Japokuwa nchi hiyo ndiyo chanzo kikubwa cha Mto Nile, Waethiopia hawaruhisiwi kuutumia mto huo katika shuguli za umwagiliaji.

Uingereza ilipokuwa msimamizi wa nchi zote za Afrika ya Mashariki, iliamuwa kuipatia Misri sehemu kubwa ya Mto Nile, kupitia makubaliano yaliyosainiwa kati ya Uingereza na Misri.

Sehemu ya Mto Nile
Sehemu ya Mto NilePicha: picture-alliance / dpa

Lakini, ukweli kwamba Mto Nile haupitii Misri tu, bali umeanzia na kupitia katika mataifa mengine ya Mashariki ya afrika, kama vile Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Tanzania, Uganda, Ethiopia, Eritrea na Sudan, unaelezea kwamba huenda mataifa hayo nayo yakahitajia kuutumia mto huo huo kwa shuguli za umwagiliaji.

Chanzo cha Mto Nile ni milima ya Ethiopia, huku ukipita maelfu ya meli kaskazini mwa Sudani na Misri kabla ya kufika bahari ya Mediterranian.

Imeripotiwa kwamba, vituo sita vya umeme vitaisaidia kuendeleza shughuli za umwagiliaji kwa wakulima nchini Ethiopia, moja kati ya nchi maskinini duniani inayohitaji sana kuwa na vyanzo vya hakika vya umeme.

Ethiopia ni miongoni mwa mataifa ya Mashariki ya Afrika yenye watu wengi ambayo pia inakabiliwa na matatizo ya maji safi ya kunywa na umeme.

Mtaalamu wa maswala ya maji wa nchi za Mashariki ya Afrika kutoka Shirika la Kimataifa la Ulinzi (SPW), Stephan Roll, ameeleza kuwa, mipango ya Ethiopia haitozuia mtiririko wa maji wa Mto Nile nchini Misri.

Misri ni nchi inayotegemea Mto Nile kwa karibuni 95% ya maji yake. Wakazi wa Misri wanatumia mto huo kwa shughuli za kilimo, kuendeshea viwanda na hata maji ya kunywa.

Tangu mwaka 1999, Misri, Ethiopia na nchi nyingine nane za jirani zimekuwa zikijadiliana juu ya haki za Mto Nile. Nchi hizi zimekuwa zikijaribu kutafuta makubaliano ya kuufanya mto huo kuwa wa pamoja, huku zikigawana faida zote, zikiwemo zile za kiuchumi na kijamii zinazopatikana kwenye mto huo. Lakini hadi sasa, hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa.

Mwaka 2010, baadhi ya nchi ziliamua kuchukua hatua zake zenyewe kuhusiana na matumizi ya Mto Nile. Ethiopia, Uganda, Rwanda, Tanzania na Kenya zilisainii makubaliano ya mfumo wa kugawana maji ya Mto Nile, huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burundi zikitegemewa kusani hapo baadaye.

Wachunguzi wameeleza kwamba makubalianao hayo yanaweza kusababisha vita hapo baadaye, ingawa wataalamu kutoka nchi hizi za Mashariki ya Afrika wanaamini hilo linaweza kuepukika.

Mwandishi: Martin Schrader

Tafsiri: Chelu Matuzya

Mhariri: Mohammed Khelef