MAFRA : Urusi na Ulaya bado zahitilafiana | Habari za Ulimwengu | DW | 27.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MAFRA : Urusi na Ulaya bado zahitilafiana

Rais Vladimir Putin wa Urusi na viongozi waandamizi wa Umoja wa Ulaya wamekuwa na mkutano wa viongozi katika mji wa Mafra nchini Ureno hapo jana wenye lengo la kutuliza uhusiano baina yao.

Miongoni mwa masuala yaliokuwemo kwenye agenda ni mzozo juu ya hatima ya baadae ya jimbo la Serbia la Kosovo na mpango wa nuklea wa Iran.Putin na Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso wameyaelezea mazungumzo hayo kuwa ya dhati na yenye tija.

Hakuna makubaliano yoyote yale makubwa yaliofikiwa na Putin ameshutumua mipango ya Umoja wa Ulaya kupunguza uwekezaji wa kigeni katika mifumo yake ya nishati.

Barroso anasema anafikiri wanaweza kujivunia ukweli kwamba uhusiano kati ya Umoja wa Ulaya na Urusi hivi sasa umetanuka zaidi na kwamba wamekuwa wakipiga hatua kubwa za maendeleo katika masuala ya kila siku yenye maslahi kwa raia zao na kwamba pia ni kweli kuna tofauti zinazoendelea kubakia lakini pia ni kweli kuwa kuna nia ya kuondokana na tofauti hizo kwa moyo mzuri wa tija na vitendo.

Hata hivyo Rais wa Urusi alivuta nadhari zaidi kwa matamshi yake juu ya mipango ya Marekani kuweka makombora ya kujihami Ulaya ya mashariki ambapo ameonya kwamba hatua hiyo inaweza kusababisha kuwepo kwa hali kama ile ya mzozo wa makombora wa Cuba wa mwaka 1962 ambapo kwayo Marekani na Urusi zilikuwa ukingoni mwa vita vya nuklea.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com